/
Modyuli ya 5: Ukusanyaji na Utayarishaji wa Sampuli ya Kipimo cha Idadi ya Virusi Kwenye Modyuli ya 5: Ukusanyaji na Utayarishaji wa Sampuli ya Kipimo cha Idadi ya Virusi Kwenye

Modyuli ya 5: Ukusanyaji na Utayarishaji wa Sampuli ya Kipimo cha Idadi ya Virusi Kwenye - PowerPoint Presentation

goldengirl
goldengirl . @goldengirl
Follow
355 views
Uploaded On 2020-11-06

Modyuli ya 5: Ukusanyaji na Utayarishaji wa Sampuli ya Kipimo cha Idadi ya Virusi Kwenye - PPT Presentation

Malengo ya Mafunzo Kujifunza aina za sampuli ya kipimo cha idadi ya virusi kwenye damu Kuelewa mchakato wa ukusanyaji wa sampuli ya damu kutoka kwa mshipa Kuelewa mchakato wa ukusanyaji wa sampuli ya damu iliyokaushwa ID: 816243

sampuli damu katika kwa damu sampuli kwa katika kwenye cha ukusanyaji iliyokaushwa kadi plazima mshipa kukataa utaratibu kutumia ili

Share:

Link:

Embed:

Download Presentation from below link

Download The PPT/PDF document "Modyuli ya 5: Ukusanyaji na Utayarishaji..." is the property of its rightful owner. Permission is granted to download and print the materials on this web site for personal, non-commercial use only, and to display it on your personal computer provided you do not modify the materials and that you retain all copyright notices contained in the materials. By downloading content from our website, you accept the terms of this agreement.


Presentation Transcript

Slide1

Modyuli ya 5: Ukusanyaji na Utayarishaji wa Sampuli ya Kipimo cha Idadi ya Virusi Kwenye Damu

Slide2

Malengo ya Mafunzo

Kujifunza aina za sampuli ya kipimo cha idadi ya virusi kwenye damu

Kuelewa mchakato wa ukusanyaji wa sampuli ya damu kutoka kwa mshipa

Kuelewa mchakato wa ukusanyaji wa sampuli ya damu iliyokaushwa

Kufafanua vipengele vya usalama katika ukusanyaji wa sampuli za damu

Slide3

Mukhtasari

Sampuli za Kipimo cha Idadi ya

Virusi

kwenye

Damu

Ukusanyaji wa Sampuli ya Damu ya Mshipa

Ukusanyaji wa Sampuli ya Damu Iliyokaushwa

Usalama katika ukusanyaji wa sampuli za damu

Slide4

Sampuli za Kipimo cha Idadi ya Virusi kwenye Damu

Aina za sampuli:

Slide5

Kutumia Sampuli ya Damu Iliyokaushwa ikilinganishwa na Plazima katika Kipimo cha Idadi ya Virusi

Sifa

Plazima

Sampuli ya Damu Iliyokaushwa

Kunahitaji kudunga mshipa wa damu

Ndiyo

Hapana

Kunahitaji mchakato wa kutenganisha kwa kutumia kifaa kinachozunguka kwa kasi

Ndiyo

HapanaThabiti katika “hali joto ya kawaida”HapanaNdiyo*Hatari kwa afya ya viumbe kwa madhumuni ya kusafirishaNdiyoHapanaBarafu kavu inahitajika katika usafirishajiNdiyoHapana*Inatumika mara kwa mara katika kuainisha jeniNdiyoHapanaKiwango cha kiasiMililita 1-5Mililita 0.25-5

*Iwapo itawekwa ikiwa kavu, kwa angalau wiki 2

Slide6

Ukusanyaji wa Sampuli ya Damu ya Mshipa

Slide7

Vifaa Vinavyohitajika katika Kukusanya Sampuli ya Damu ya Mshipa

Vichupa vya gilasi ambavyo huwekwa damu iliyotolewa kwenye mishipa

Sindano inayoingizwa kwenye kichupa cha kuweka damu na kifaa cha kushikilia sindano

Tyubi za barafu (Nunch)

Glavu zisizo na poda

Vitambaa vya kupagusa vyenye alkoholi

Sifonjo za shashi

Kifaa cha kubana mshipa ili iwe rahisi kutoa damu

Bendeji

Mkebe wa kuweka vitu vyenye makaliKalamu ya kuweka alama yenye wino wa kudumu

Slide8

Sampuli ya Damu ya Mshipa -

Ukusanyaji

Ukusanyaji wa sampuli ya damu unapaswa kufanywa kwa kutumia glavu zisizo na poda.

Damu inapaswa kukusanya kwa kutumia tyubu safi kwa kutumia EDTA (kifuniko cha zambarau) pekee.

Kusanya takriban mililita 5 za sampuli ya damu ukitumia tyubu ya kuweka damu ya EDTA kutoka kwa wagonjwa wote ambao ni watu wazima.

Sampuli inapaswa kutumwa kwa kituo au maabara ya kufanyia upimaji ndani ya masaa 24 (kwa kawaida ndani ya masaa 6) baada ya kukusanywa ili kutenganisha plazima kutoka kwa damu kwa kuzungusha.

Slide9

Sampuli ya Damu ya Mshipa -

Uchakataji

Tenganisha plazima kwa mchakato wa kuzungusha kwa kasi kwa 800-1600x g kwa dakika 20 au 2450x g kwa dakika 10 katika hali joto ya kawaida.

Hamisha plazima hadi kwenye tyubu ya polipropilini (Cryo). Kuwa makini usivuruge ganda lenye rangi ya manjano ili kuzuia uchafuzi kutoka kwa chembechembe za seli.

Hamisha kiasi kidogo cha sampuli ya mililita 1.2 au maikrolita 1200 hadi kwa kila tyubu ya polipropilini yenye lebo.

Hakikisha kuwa tyubu za polipropilini zimefunikwa vizuri.

Slide10

Sampuli ya Damu ya Mshipa -

Uhifadhi

Uchakataji wa sampuli na kituo cha kuhifadhi kinahitaji kuwa na vifaa na zana za kutumia zinazofaa.

Hifadhi plazima katika nyuzijoto 2-8

hadi siku 5, au kwenye barafu ya nyuzijoto -20 hadi -70

au baridi zaidi.

Sampuli za plazima zinaweza kuhifadhiwa kwa hadi masaa 24 kwenye nyuzijoto 15-30 15-30 .Sampuli za plazima huhifadhiwa katika nyuzijoto -70  iwapo zinahitaji kuhifadhiwa kwa muda mrefu.Muda wa KuhifadhiAina ya sampuli:Hali joto ya kuhifadhiNyuzijoto 37Nyuzijoto 15-30Nyuzijoto 4Nyuzijot0 -20Nyuzijoto -70

Damu yote

Masaa 24

Masaa 24

Haitumiki

Haitumiki

Haitumiki

Plazima

Masaa 24

Masaa 24

Siku 5

Mwaka

1

Miaka

5

Slide11

Sampuli ya Damu ya Mshipa -

Usafirishaji

Sampuli zinapaswa kulindwa kutokana na uharibifu, joto na kuvurugwa.

Dumisha uaminifu wa sampuli:

Sampuli ya damu yote lazima isafirishwa katika nyuzijoto 2-25

na ichakatwe ndani ya masaa 24 baada ya kukusanywa.

Plazima inaweza kusafirishwa katika nyuzijoto 2-8

, au katika hali ya kugandishwa kwa barafu kwa nyuzijoto -20 hadi -70  ikiwa tayari imegandishwa.Hakikisha kanuni za usalama zimetimizwa.Upakiaji mara tatu

Slide12

Kufunganya katika Vifurushi Vitatu

Slide13

Sampuli ya Damu ya Mshipa -

Utaratibu

wa

Kukataa

Kiasi cha sampuli kisichotosha

Sampuli imeganda

Sampuli zenye chembechembe nyingi za mafuta na seli nyekundu za damu

Uwezekano wa kuwa imechafuliwa

Utenganishi mbaya wa plazimaSampuli za Plazima HAZITENGANISHWI ndani ya masaa 24 baada ya kukusanywa Sampuli zilizokusanywa kwa kutumia kemikali za kuzuia kuganda kwa damu ambazo si za EDTA (HEPARIN au ACD)Sampuli za plazima ambazo HAZIJAWEKWA kwa barafu kwa zaidi ya siku 5 kabla ya kupimwaSampuli za plazima zimewekwa kwenye barafu na kurudishwa katika hali joto ya kawaida kwa zaidi ya mara 5 kabla ya kupimwaSampuli za plazima haijahifadhiwa katika hali joto inayofaa kwatai usafirishajiTyubu za sampuli zisizo na lebo au zenye lebo ambayo haisomekiFomu ya maabara ya kuomba sampuli haipo

Slide14

Sampuli ya Damu ya Mshipa -

Utaratibu

wa

Kukataa

Umajimaji wa damu na plazima inayoweza kutumiwa

Yenye chembechembe nyingi za mafuta

Iliyochafuliwa

Yenye chembechembe nyingi ya seli nyekundu za damu

Slide15

Ukusanyaji wa Sampuli ya Damu Iliyokaushwa (DBS)

Slide16

Vifaa Vinavyohitajika katika Ukusanyaji wa Sampuli ya Damu ya Iliyokaushwa

Glavu (zisizo na poda)

Kadi ya 903 ya Whatman ya kutumika wakati wa ukusanyaji

Sehemu ya kukaushia kadi

Kifaa cha kudunga ngozi kinachojirudisha baada ya kuchukua sampuli ya damu

Vitambaa vya kupagusa vyenye alkoholi

Shashi kavu iliyo safi

Kifurushi cha kukausha

Kadi za kuashiria unyevunyevu

Mifuko ya plastiki inayofungwa kwa zipu na isiyoingiza unyevunyevuWino wa kuweka lebo usiosafishwa na majiKaratasi ya rangi ya kutumiwa kwa vifaa vya glasi (karatasi ya kupimia uzito)Mfuko wa kuweka uchafu unaoewa kudhuru viumbe unaowekwa juu ya meza na kifaa cha kuushikiliaMkebe wa kuweka vitu vyenye makaliKalamu

Slide17

Ukusanyaji wa Sampuli ya Damu Iliyokaushwa (DBS)

Tumia tahadhari za jumla za usalama

Matumizi ya kadi za sampuli ya damu iliyokaushwa zilizokubaliwa, zenye mashimo

umependekezwa

sana

Weka lebo wazi kwa kila kadi kwa kutumia nambari ya utambulishi

Ukusanyaji wa sampuli ya damu unapaswa kufanywa kwa kutumia glavu zisizo na poda

Damu inaweza kukusanywa kwa kudunga kidole au kisigino au kutoka kwa mshipa kwa kutumia tyubu safi kwa kutumia EDTA (kifuniko cha rangi ya zambarau)

Ikiwa inahitajika, damu ambayo haijaganda kwa kukusanywa na EDTA inaweza kuhifadhiwa kwa hadi masaa 24, kabla ya kutayarishwa kwa sampuli ya damu iliyokaushwa, ikiwezekana kwenye nyuzijoto 4

Weka matone 5 ya damu kwenye kadi ya sampuli ya damu iliyokaushwa, au utumie kidodez ili kuhamisha damu kwa sampuli zinazokusanywa kutoka kwa mshipa.

Slide18

Vidokezo vya Ukusanyaji wa Sampuli ya Damu Iliyokaushwa (DBS)

Usiguse

sehemu za kadi ambazo zitatumika kukusanya sampuli haijalishi kama umevaa glavu

au

haujavaa.

Usipake

damu kwenye sehemu zote mbili za karatasi ya kuchuja.

Usipake damu

zaidi ya mara moja katika duara sawa ya kukusanyia.

Usipake damu kutoka kwa zaidi ya mgonjwa mmoja katika kadi sawa ya kukusanyia.Usifinyilie karatasi ya kuchuja kwenye sehemu iliyodungwa ili kutoa damu.Usijaribu “kukamua” kidole.

Slide19

Sampuli ya Damu Iliyokaushwa (DBS) -

Uhifadhi

Sampuli ya Damu Iliyokaushwa (DBS) inapaswa kukaushwa kwa hewa kabla ya kupakiwa, kwa kawaida kwa masaa 4 au usiku kucha.

Sampuli inapaswa kuhifadhiwa katika mifuko ya plastiki inayofungwa na zipu na isiyoingiza hewa ikiwa na kemikali za kuausha na kadi za kuashiria unyevunyevu.

Epuka kuhifadhi kadi za sampuli ya damu iliyokaushwa katika hali joto ya kawaida kwa zaidi ya wiki moja.

Epuka kupigisha sampuli miale ya jua na joto moja

kwa

moja.

Kadi zinapaswa kuwekwa lebo yenye vitambulishi vinavyofaa.

Slide20

Sampuli ya Damu Iliyokaushwa (DBS) -

Usafirishaji

Dumisha uaminifu wa sampuli

Ufuatiliaji wa hali joto wakati wa usafirishaji

Fuatilia hali ya kiashiria cha unyevunyevu

Kizuizi cha muda

Hakikisha kanuni za usalama zimetimizwa

Shughulikia sampuli za damu iliyokaushwa kama vifaa vinavyoweza kudhuru viumbe hai (lakini hazina haja ya kufunganywa kwa kutumia vifurushi vitatu)

Slide21

Sampuli ya Damu Iliyokaushwa (DBS): Sampuli Inayokubalika

Taarifa ya utambulishi

kwenye kadi ya sampuli ya damu uliyokaushwa inapaswa kuwa wazi na ilingane na hati zinazoambatana nayo.

Ni lazima

angalau matone 3 mazuri

yachukuliwe.

Sampuli zinapaswa kujaza miduara na ziwe katikati iwezekanavyo, hasa katika kadi zenye mashimo.

Baada ya kukaushwa, sampuli ya damu ya matone inapaswa kuwa

nyeusi na yenye rangi sawa,

kuonyesha kuwa imekusanywa na kukaushwa kwa mbinu inayofaa.

Slide22

Sampuli ya Damu Iliyokaushwa (DBS): Utaratibu wa Kukataa Sampuli

Kiasi cha sampuli kisichotosha/miduara isiyokamilika

Sampuli iliyoganda

Yenye seli nyekundu zilizoharibiwa/mzingo wa umajimaji wa damu

Iliyochubuka/kukwaruzwa

Ambayo haijakauka/funganywa kabla ya kukauka

Udhibiti mbaya wa unyevunyevu

Sampuli isiyo na lebo au yenye lebo ambayo haisomeki

Sampuli au fomu ya maabara ya kuomba sampuli haipo

Slide23

Utaratibu wa Kukataa Sampuli:

Kitambulishi Hakisomeki

Tatizo:

Maelezo kwenye Kitambulisho hayasomeki, kwa hivyo sampuli haipaswi kupimwa

Slide24

Utaratibu wa Kukataa Sampuli:

Kitambulishi Hakisomeki

Suluhu:

Weka lebo kwenye kadi ya sampuli ya matone ya damu yaliyokaushwa kabla ya kuchukua sampuli

Iwapo jina halisomeki, sampuli nyingine inahitajika

Slide25

Utaratibu wa Kukataa Sampuli:

Kiasi cha Damu Kisichotosha

Tatizo:

Matone haya hayana damu inayotosha kupimwa.

Kumbuka, angalau MATONE 3 MAZURI yanahitajika ili kupimwa.

Slide26

Utaratibu wa Kukataa Sampuli:

Kiasi cha Damu Kisichotosha

Suluhu:

Iwapo sampuli inachukuliwa kutoka kwa kidole au kisigino, kuhakikisha sehemu hiyo ina joto na imewekwa vizuri kutasaidia damu kutoka vizuri ili sampuli ichukuliwe.

Usikamue sehemu iliyodungwa, finya mkono au mguu wote.

Iwapo damu imeacha kutoka kwenye sehemu uliyodunga, kuna haja ya kudunga mara ya pili sehemu tofauti na ya kwanza.

Mtu mgonjwa au asiye na maji ya kutosha kwa mwili atahitaji kudungwa mshipa ili kutoa damu.

Hakikisha kwamba kidodezi kimekwa kwenye kiasi cha

maikrolita

70.

Slide27

Utaratibu wa Kukataa Sampuli:

Damu Iliyoshikana au Kuganda

Matatizo:

Tambua kuwa matone ni meusi zaidi katikati. Hii hutokea iwapo umekwa damu ambayo haijakauka juu ya damu iliyokauka.

Hii inaweza kuwa ilitokea kwa sababu ya kutumia damu iliyoganda.

Slide28

Utaratibu wa Kukataa Sampuli:

Damu Iliyoshikana au Kuganda

Suluhu:

Gusisha kadi kwenye tone la damu linapoonekana kuwa nzito na linakaribia kuanguka. Hiki ndicho kiasi

sawa

cha

damu.

Ikiwa tone ni dogo sana, na bado halijakauka, tone lingine linaweza kuwekwa juu ya hilo. La sivyo, enda kwenye

tone

lingine.Kamwa usitumie damu inayoganda au iliyoganda ili kutengeneza sampuli ya matone ya damu yaliyokauka.

Slide29

Utaratibu wa Kukataa Sampuli:

Miduara ya umajimaji wa damu/Damu Iliyochafuliwa na Vileo

Matatizo:

Uzingo wa rangi ya manjano unaozunguka matone ya damu unamaanisha kuwa damu imechafuliwa au kutenganishwa.

Alkoholi inaweza kuwa haikukauka.

Hii inaweza kutokea kwa sababu ya kufinya sehemu iliyodungwa ili kutoa damu - plazima inaweza kutoka badala ya damu.

Pia inaweza kuwa kwa sababu ya kukosa kuchanganya tyubu ya EDTA kabla ya kutengeneza matone.

Slide30

Utaratibu wa Kukataa Sampuli:

Miduara ya umajimaji wa damu/Damu Iliyochafuliwa na Vileo

Suluhu:

Baada ya kusafisha sehemu ya kutoa damu, hakikisha alkoholi inakauka kwa sekunde 30 kabla ya kutoa damu au kudunga.

Finya kwa upole mkono au mguu wote ili kuwezesha damu kutoka. Kamwe “usikamue” au kufinya sehemu iliyodungwa moja kwa moja.

Ikiwa unatengeneza sampuli za matone ya damu yaliyokaushwa kutoka kwa tyube ya EDTA, hakikisha umegeuza tyubu ili kuchanganya damu mara kadhaa kabla ya kuihamisha na kidodezi.

Slide31

Utaratibu wa Kukataa Sampuli:

Damu Nyingi

Matatizo:

Kuna uwezekano damu hii iliwekwa kwa sindano au kidodezi ambacho hakijawekwa kiasi kinachofaa.

Damu imevuja hadi ile sehemu nyingine ya kadi.

Slide32

Utaratibu wa Kukataa Sampuli:

Damu Nyingi

Suluhu:

Tumia tyubu ya EDTA ili kutoa damu

kwenye

mshipa.

Tumia kidodezi kilichowekwa kiasi kinachofaa ili kutengeneza sampuli ya matone yaliyokaushwa.

Usijaze sana.

Slide33

Utaratibu wa Kukataa Sampuli:

Mbinu Isiyofaa ya Ukusanyaji

Matatizo:

Kuna uwezekano damu ilikuwa inaendelea kuganda wakati matone yalipowekwa kwenye kadi.

Zaidi ya tone moja iliwekwa kwenye mduara.

Hakuna mduara wowote uliojazwa damu ipasavyo.

Slide34

Utaratibu wa Kukataa Sampuli:

Mbinu Isiyofaa ya Ukusanyaji

Suluhu:

Subiri hadi tone kubwa likusanyike kabla ya kugusisha damu kwenye karatasi.

Tone la damu linalomwagika bila kuguswa ndilo kiasi kinachofaa.

Usigusishe karatasi kwenye ngozi, sindano, sirinji, au ncha ya kidodezi unapoweka damu.

Slide35

Usalama katika Ukusanyaji wa Sampuli

za

Damu

Slide36

Usalama katika Ukusanyaji wa Sampuli

za

Damu

Watu wote wanaoshughulikia sampuli za damu katika hatua yoyote ya ukusanyaji, uchakataji na usafirishaji ni lazima wafuate mitindo sanifu ya usalama ya kushughulikia bidhaa za mwili zenye uwezo wa kuleta maambukizi.

Upunguzaji wa hatari ya maambukizi kutokana na bidhaa za mwili unawezekana kupitia mchanganyiko wa mitindo na mienendo salama, vituo salama, na zana salama ambazo zinawezesha kudhibiti uhifadhi wa bidhaa zinazoweza kuambukiza.

Taratibu sanifu za ushughulikiaji unaotolewa na Huduma za Maabara za Kitaifa (National Laboratory Services) za matumizi ya vifaa vya ulinzi wa mtu binafsi, usafishaji wa vifaa vinavyotumiwa tena kama vile masanduku ya barafu, na usafishaji na utupaji wa bidhaa hatari za mwili zilizomwagika na zilizotumika zinapaswa kufuatwa.

Slide37

Usalama katika Ukusanyaji wa Sampuli

za

Damu

Katika tukio ambapo sampuli itamwagika bila kukusudia, anayeisafirisha anapaswa kushughulikia umwagikaji kwa kutumia taratibu sanifu za kudhibiti bidhaa hatari

za

mwili.

Iwapo kuna uwagikaji au uchelewashaji wakati wa usafirishaji, ripoti ya tukio inapaswa kujazwa kwenye Fomu ya Ufuatiliaji wa Sampuli kwa ajili ya uthibitishaji wa ubora.

Wahudumu wa kliniki wanaoshughulikia usafirishaji wa sampuli wanapaswa kufuata taratibu zinazofaa za ushughulikiaji wa mchakato huo.

Slide38

Una Maswali?

Related Contents


Next Show more