Malengo ya Mafunzo Kutoa mafunzo ya kisaikolojia kwa njia zinazoendeleza mabadiliko ya tabia Kuelewa vielelezo vya mabadiliko ya tabia Kuelewa masuala ya kawaida ya tabia na hisia yanayochangia kuwepo na ugumu katika kuzingatia matibabu yafaayo ya kudhibiti virusi ART ID: 805010
Download The PPT/PDF document "Mafunzo ya Kiwango cha Juu ya Utoaji Ush..." is the property of its rightful owner. Permission is granted to download and print the materials on this web site for personal, non-commercial use only, and to display it on your personal computer provided you do not modify the materials and that you retain all copyright notices contained in the materials. By downloading content from our website, you accept the terms of this agreement.
Slide1
Mafunzo ya Kiwango cha Juu ya Utoaji Ushauri
Slide2Malengo ya Mafunzo
Kutoa mafunzo ya kisaikolojia kwa njia zinazoendeleza mabadiliko ya tabia
Kuelewa vielelezo vya mabadiliko ya tabia
Kuelewa masuala ya kawaida ya tabia na hisia yanayochangia kuwepo na ugumu katika kuzingatia matibabu yafaayo ya kudhibiti virusi (ART)
Kujifunza sababu za ukuaji wa akili zinazochangia katika ugumu wa kuzingatia matumizi yafaayo ya dawa
Kujifunza stadi mahususi za malezi na watoto ambazo ni muhimu katika kutoa ushauri wa uzingatiaji wa matumizi yanayofaa ya dawa kwa wazazi na watoto
Slide3Mukhtasari
Kielelezo cha Mafunzo ya Kiwango cha Juu ya Utoaji Ushauri
Sehemu ya 1: Mabadiliko Makubwa ya Tabia
Kufikia Watu Katika Hali Zao: Hatua za Mabadiliko
Mazungumzo ya Kuhimiza Mabadiliko
Faida na Hasara
Sehemu ya 2: Mambo ya Kuzingatia katika Ukuaji
Ukuaji wa Vijana na Uzingatiaji wa Matumizi Yafaayo ya Dawa
Uzingatiaji wa Dawa wa Watoto: Kufanya Kazi Watunzaji
Slide4Mabadiliko Makubwa ya Tabia
Slide5Kielelezo cha Mabadiliko:
Kufikia Watu Katika Hali Zao
Slide6Kielelezo cha Mabadiliko:
Kufikia Watu Katika Hali Zao
Kabla ya Kutafakari
Kuona kuwa hakuna haja ya badiliko la mtindo wa maisha au tabia
Kwa mfano: “Kila mtu huniambia nitumie dawa zangu za kudhibiti VVU, lakini sina uhakika ninazihitaji. Ninahisi vizuri hata bila kuzitumia.”
Jukumu la mshauri: tumia ukosefu wao wa uhakika kutoa ushauri.
“Ninasikia unasema kuwa hauna ukahika ikiwa unahitaji dawa za kudhibiti VVU hata kama unajihisi vizuri. Ni nini kinakufanya ufikiri kuwa utazihitaji?”
“Iwapo unajihisi vizuri, ni kwa nini watu hukwambia ni muhimu kuendelea kutumia dawa za kudhibiti VVU?”
Slide7Kielelezo cha Mabadiliko:
Kufikia Watu Katika Hali Zao
Kutafakari
Kutafakari kufanya badiliko lakini bado hakuna maamuzi
Kwa mfano: “Ninafikiri ninapaswa kuanza kutumia dawa zangu za kudhibiti VVU.”
Jukumu la mshauri: himiza uamuzi wao wa kubadilika
“Ikiwa utaanza kutumia dawa za kudhibiti VVU, unafikiri ni nini kitakuwa bora?”
“Ni nini kinakufanya huhisi kuwa sasa ndio muda bora wa kuanza kutumia dawa za kudhibiti VVU?”
Slide8Kielelezo cha Mabadiliko:
Kufikia Watu Katika Hali Zao
Matayarisho
Ameamua kufanya mabadiliko na anatafakari jinsi ya kuyafanya
Kwa mfano: “Sawa, ninajua ninahitaji kutumia dawa zangu za kudhibiti VVU, ingawa huwa nasahau. Labda ninaweza kufanya jambo la kunisaidia kukumbuka.”
Jukumu la mshauri: saidia kufanya mpango wa mabadiliko
“Wakati ambapo ulikumbuka kutumia dawa zako za kudhibiti VVU hapo nyuma, ni nini kilikusaidia?
“Una vifaa gani vya kukusaidia kukumbuka kutumia dawa za kudhibiti VVU?”
Slide9Kielelezo cha Mabadiliko:
Kufikia Watu Katika Hali Zao
Hatua
Kufanya jambo halisi ili kuleta badiliko
Kwa mfano: “Nitaweka kengele ya saa ili nijikumbushe kutumia dawa za kudhibiti VVU.”
Jukumu la mshauri: unga mkono hatua hiyo
“Umechagua hatua zuri ya kwanza. Tunaweza kuweka kengele hiyo sasa hivi?”
“Je, unafikiri ni nini kinaweza kuzuia hatua hiyo isifanikiwe?”
“Je, utahisiaje ukifanya badiliko hilo?”
Slide10Kielelezo cha Mabadiliko:
Kufikia Watu Katika Hali Zao
Udumishaji
Kufanya juhudi za kudumisha badiliko au mtindo mpya wa maisha. Majaribu na kurudi nyuma ni mambo ya kawaida.
Kwa mfano: “Wakati mwingine hupatwa na majaribu ya kusema ‘nitameza dawa zangu za kudhibiti VVU baadaye’ badala ya kuzimeza wakati ninaposiki kengele ya saa ya kunikumbusha. Wakati mwingine huwa nina shughuli nyingi sana.”
Jukumu la mshauri: unga mkono na utoe mpango
“Ni vigumu kuendelea na mabadiliko haya. Je, unafikiri unaweza kufanya nini ili kuendelea nayo hata wakati kuna mambo mengine ambayo ni muhimu zaidi kwako?”
“Wakati ujao utakapofikiri ‘nitameza dawa zangu za kudhibiti VVU baadaye,’ unaweza kufanya nini tofauti?”
Slide11Kielelezo cha Mabadiliko:
Kufikia Watu Katika Hali Zao
Kuzorota kwa kurudi katika hali ya awali
Ni jambo la kawaida na vipindi vya kurudia tabia ya awali. Kuelewa kuwa hili ni jambo la kawaida husaidia katika kurudia tabia ya sasa ya kubadilika bila aibu au kuhisi umekosea.
Kwa mfano: “Nilianza kupuuza kengele ya saa yangu kwa sababu nilikuwa na shughuli nyingi sana hadi mwishowe nikaizima.”
Jukumu la mshauri: thibitisha na ukadirie utayari
“Ni vigumu sana kuendelea na mabadiliko haya. Je, unahisiaje kuhusu kuanza tena kutumia dawa za kudhibiti VVU sasa?”
Slide12Kielelezo cha Mabadiliko:
Kufikia Watu Katika Hali Zao
Slide13Mazungumzo ya Mabadiliko: Hatua
Slide14Faida
Hasara
Kubadilika
Faida za Kubadilika
Hasara za Kubadilika
Kutobadilika
Faida za
Kutobadilika
Hasara za
Kutobadilika
Kielelezo cha Mabadiliko:
Kufikia Watu Katika Hali Zao
Faida na Hasara
Slide15Faida
Hasara
Kubadilika
Faida za Kuanza Kutumia Dawa za Kudhibiti VVU:
Afya bora kwa muda mrefu, kupungua kwa hatari ya usambazaji
Hasara za Kubadilika:
Kutembelea hospitali mara nyingi katika siku za mwanzo, athari zinazotokana na kutumia dawa
Kutobadilika
Faida za
Kutobadilika
Kuendelea kutumia muda/nguvu kwa mambo ya kazini/nyumbani/familia
Hasara za
Kutobadilika
Matokeo mabaya ya afya, hatari kubwa ya usambazaji
Kielelezo cha Mabadiliko:
Kufikia Watu Katika Hali Zao
Faida na Hasara
Slide16Una Maswali?
Slide17Mambo ya Kuzingatia katika Ukuaji
Slide18Ni nini Kinahitajika ili Kuwa na Uzingatiaji “Mzuri”
UZINGATIAJI MZURI
Umakini
Shughuli Yenye Nia ya Kutimiza Lengo Fulani
Kuelewa
Masuala ya Afya
Kuwa na Mpango
Kutatua Tatizo
Kudhibiti Hisia
Kujikazia ili Upate Faida Hapo Baadaye
Kuwa na Mpango
Kumbukumbu
Uwezo wa Kudhibiti Mambo Yanayokengeusha
UZINGATIAJI MZURI
Motisha
Jambo Lingine Lolote?
Slide19Kinahitajika ili Kuwa na Uzingatiaji “Mzuri”
Kazi za Gamba la Mbele la Ubongo
Kupanga
Kutimiza Shughuli
zenye
Lengo Fulani
Kutia Motisha
Kuelewa Masuala ya Afya
Umakini
Kutatua Tatizo
Kudhibiti HisiaKujikazia ili Upate Faida Hapo BaadayeKumbukumbuUwezo wa Kudhibiti Mambo Yanayokengeusha
Slide20Ukuaji wa Gamba la Mbele la Akili
Slide21Kufanya Kazi na Ukuaji
Saidia
Boresha
Slide22Uzingatiaji Miongoni mwa Vijana:
Kuongoza Matumizi ya Dawa Zako za Kudhibiti VVU
Slide23Uzingatiaji Miongoni mwa Vijana:
Kuongoza Matumizi ya Dawa Zako za Kudhibiti VVU
“Ni wewe tu unayeishi kwenye mwili wako - ni jukumu lako kuhakikisha unatumia dawa za kudhibiti VVU ili kuulinda.”
“Watu wengi hupata msaada wa kutumia dawa za kudhibiti VVU, lakini hatimaye ni jukumu lako.”
Ubadilishaji wa jukumu
Uzingatiaji Miongoni mwa Vijana:
Kuongoza Matumizi ya Dawa Zako za Kudhibiti VVU
“Je, ni nani anajua kuwa
una
VVU?”
“Je, ni nani anaweza kuwa msaada kwako unapodhibiti hali yako
ya
VVU?”
Ubadilishaji wa Jukumu
Usaidizi na Ufichuaji
Slide25Uzingatiaji Miongoni mwa Vijana:
Kuongoza Matumizi ya Dawa Zako za Kudhibiti VVU
“
Ninasikia ukisema kwamba una mabadiliko mengi sana hivi sasa katika maisha yako, je, unafikiri hili linaweza kuathiri aje matumizi yako ya dawa za kudhibiti VVU?
“Unaishi wapi? Unaishi na nani? Hili linaweza kuathiri aje matumizi yako ya dawa za kudhibiti VVU?”
“Ni nani anayekusaidia kutumia dawa zako kwa sasa? Je, unafikiri jambo hili linaweza kubadilikaje katika siku za usoni?
Usaidizi na Ufichuaji
Mabadiliko katika Maisha
Slide26Uzingatiaji Miongoni mwa Vijana:
Kuongoza Matumizi ya Dawa Zako za Kudhibiti VVU
“Inaonekana una shughuli nyingi kweli! Ninasikia ni muhimu kwako kuwa na afya njema ili kuendelea na shughuli hizi. Je, unafikiri kutumia dawa za kudhibiti VVU zitaingiaje kwenye ratiba yako?”
Mabadiliko katika Maisha
Ratiba Zinazobadilikabadilika
Slide27Uzingatiaji Miongoni mwa Vijana:
Ni Nani Unapaswa Kuambia na ni Kwa Nini
Slide28Uzingatiaji Miongoni mwa Vijana:
Ni Nani Unapaswa Kuambia na ni Kwa Nini
Tumia chupa ya tembe isiyo na alama ya kukutambulisha.
Tumia visanduku vya tembe badala ya chupa.
Fikiria kuhusu mahali amapo unaweza kuweka dawa na ambapo hazitaonekana na watu wengine lakini wewe utaziona
kila
siku.
Njia za Kulinda Faragha
Slide29Uzingatiaji Miongoni mwa Vijana
U
napaswa kuambia nani na ni kwa nini
“Je, unafikiri ni sifa gani ambazo ni za chaguo zuri la mtu kushiriki
hali
yake?”
“Je, kuna faida gani kwa mtu mwingine kujua hali yako?”
“Je, unaamuaje iwapo unaweza kumwamini mtu?”
“Je, unamwambiaje mtu hali yako?”
“Je, una wasiwasi kuwa utapata madhara iwapo utafichua hali yako
ya VVU?”
Jadili Njia za Kuamua ni Nani wa Kushiriki Utambuzi Naye na Lini Kufanya Hivyo
Slide30Uzingatiaji Miongoni mwa Vijana:
Ni nani unapaswa kuambia na ni kwa nini
“Je, unafikiri itakuwaje kumwambia mpenzi wako kuhusu hali yako
ya
VVU?”
“Je, ni nini kitakuwa faida kwa mpenzi wako iwapo unatumia dawa zako za kudhibiti VVU kila siku?”
“Je, unafikiri mpenzi wako atakusaidiaje kutmia dawa zako za kudhibiti VVU?”
Ikiwa Mtu ako katika Uhusiano
Slide31Uzingatiaji Miongoni mwa Watoto:
Kufanya Kazi na Watunzaji
Slide32Uzingatiaji Miongoni mwa Watoto:
Jukumu la Mtunzaji
Ni jukumu la mtu mzima kumpa mtoto dawa za kudhibiti VVU
Angazia sababu zinazomfanya mtunzaji atake mtoto awajibike
Je, ni zipi baadhi ya sababu ambazo wazazi hukwambia?
Je, unawezaje kutumia stadi ambazo tumezungumzia leo kumsaidiza mtunzaji?
Slide33Uzingatiaji wa Dawa Miongoni mwa Watoto:
Kuzungumza na Mtoto wako kuhusu Dawa za Kudhibiti VVU
Mambo Muhimu ya Kufunza Watunzaji
Ni jambo la kawaida kwa watoto kuwa wadadisi.
Ni muhimu kuwaambia watoto ukweli.
Utakachosema, ikiwa ni pamoja na lini utakapowaambia kuhusu VVU, kitategemea umri wao na jinsi wanavyoweza kuelewa vizuri.
Maswali ya Kuzingatia
Je, wameshiriki nini kufikia sasa?
Je, mtoto wao ameuliza maswali gani?
Je, wana wasiwasi gani kuhusu
kushiriki?Je, mtunzaji anaweza kufikiri ni nini kinachoweza kusaidia?
Slide34Uzingatiaji wa Dawa Miongoni mwa Watoto:
Watoto Kukataa Kutumia Dawa
Uliza
“Wakati mwingine inaweza kuwa vigumu kuwapa watoto dawa.
Je, unafikiri mtoto wako anakataa kwa nini?”
Slide35Uzingatiaji wa Dawa wa Watoto:
Mtoto Kukataa Kutumia Dawa na Jinsi ya Kumhimiza Azitumie
Slide36Uzingatiaji wa Dawa Miongoni mwa Watoto:
Mtoto Kukataa Kutumia Dawa na Jinsi ya Kumhimiza Azitumie
Adhabu hupunguza
tabia ya kubadilika.
Uhimizaji huzidisha
tabia ya kubadilika.
Kutumia dawa ni stadi tunayotaka
iendelee
.
Stadi hukua kwa sababu ya uhimizaji,
sio adhabu.Watoto wanaotumia dawa ili kuepuka adhabu hawatakuza stadi za kujitegemea na watakuwa na ugumu kudhibiti ugonjwa wao wakati wa kipindi cha ujana na utu uzima.
Slide37Uzingatiaji wa Dawa Miongoni mwa Watoto:
Mtoto Kukataa Kutumia Dawa na Jinsi ya Kumhimiza Azitumie
Kutia Motisha
“Unafanya kazi zuri kudumisha afya njema!”
“Ninajivunia kuwa unakumbuka kutumia dawa zako bila kusaidiwa!”
Kumsifu akisikia: Ambia mtu kuhusu tabia zuri ya mtoto wako wakiwa karibu ili wasikie.
Njia zingine za kumhimiza zinaweza kujumuisha kitu cha kuchezea, muda wa ziada wa kucheza, ama peremende anayotaka
Weka kanuni za kufuata:
Kwanza meza dawa, kisha ucheze.
Ficha ladha ya dawa:
Changanya dawa kwenye kijiko kidogo cha asali au jemu.Peana dawa pamoja na peremende.
Slide38Uzingatiaji wa Dawa Miongoni mwa Watoto:
Mtoto Kukataa Kutumia Dawa na Mwongozo wa Chati cha Kibandiko
Watunzaji wanapaswa kuunda chati na watoto wao
Vibandiko vinapaswa kupeanwa punde tu baada ya tabia
inayotakikana
kutokea
Tabia inapaswa kuwa wazi:
Kibandiko cha kutumia dawa za kudhibiti VVU
Kibandiko cha kukosa kubishana
Kibandiko cha kukumbuka bila kusaidiwa
Sifa au vibandiko mara nyingi huwa vinatosha kuhimiza mtotoIkiwa uhimizaji zaidi unatumika, unapaswa kuwa mdogo na uchaguliwe kwa kumhusisha mtoto (chaguo la tamutamu, muda wa ziada wa kucheza, kifaa cha kucheza nacho)Malengo yanapaswa kuwa ambayo yanaweza kufanyika:Mtoto anayebishana kila siku kuhusu dawa anapata burudani mwishoni mwa wiki ikiwa alitumia dawa kwa siku 3 bila kubishana.Mtoto mdogo asitarajiwe kukumbuka kutumia dawa za kudhibiti VVU bila
usaidizi.
Slide39Mukhtasari: Kuunga Mkono Mabadiliko ya Tabia
Ni muhimu kuelewa sababu zote mbili za kitabia na kihisia zinazoleta matatizo ya kuzingatia matumizi yafaayo ya dawa
Vijana wanapitia kipindi maalum cha ukuaji kinachohitaji watoaji huduma kuwapa usaidizi na wakati huo huo kujenga stadi wanazohitaji ili wajitunze wao wenyewe
Watoaji huduma ni lazima wafanye kazi na wazazi ili kutafuta suluhu zitakazowawezesha kumpa mtoto wao dawa za kudhibti virusi (ARV) kila siku
Slide40Uigizaji: Kushauri Kijana
Mshiriki wa A: Mtoaji Huduma
Mshiriki wa B: Joseph
Ana umri wa miaka 16
Aliambukizwa VVU akiwa mtoto mchanga
Huudhika kwa kuwa inamlazimu kutumia dawa za kudhibiti virusi na mara nyingi husahau kuzitumia wakati wa asubuhi, hivyo kukosa kipimo cha siku hiyo
Hajamwambia rafiki yake yeyote kwamba ana VVU na anataka kuanza urafiki wa kimapenzi
Slide41Uigizaji: Kushauri Mzazi wa Mtoto Aliye
na
VVU
Mshiriki wa A: Sarah
Mamaye Elizabeth, ana miaka 7
Elizabeth ana shida za kumeza tembe na hukasirika wakati wa kuzimeza
Sara anahisi kuwa amelemewa na mara nyingi hukasirishwa na Elizabeth kwa sababu ya kusumbuka kutumia dawa zake za kudhibiti VVU kila siku.
Kwa kawaida Elizabeth hufuata maagizo vizuri, hasa akiahidiwa kuruhusiwa muda wa ziada wa kucheza
Mshiriki wa B: Mtoaji Huduma
Slide42Una Maswali?