/
WATU WA MUNGU WALIOTIWA MUHURI WATU WA MUNGU WALIOTIWA MUHURI

WATU WA MUNGU WALIOTIWA MUHURI - PowerPoint Presentation

mjnt
mjnt . @mjnt
Follow
346 views
Uploaded On 2020-09-29

WATU WA MUNGU WALIOTIWA MUHURI - PPT Presentation

Somo la 6 kwa ajili ya Februar i 9 2019 Nikamwambia Bwana wangu wajua wewe Akaniambia Hao ndio wanatoka katika dhiki ile iliyo ID: 812614

kwa katika kondoo mungu katika kwa mungu kondoo muhuri mwana kama ufunuo watu 000 yao 144 wala kila ambao

Share:

Link:

Embed:

Download Presentation from below link

Download The PPT/PDF document "WATU WA MUNGU WALIOTIWA MUHURI" is the property of its rightful owner. Permission is granted to download and print the materials on this web site for personal, non-commercial use only, and to display it on your personal computer provided you do not modify the materials and that you retain all copyright notices contained in the materials. By downloading content from our website, you accept the terms of this agreement.


Presentation Transcript

Slide1

WATU WA MUNGU WALIOTIWA MUHURI

Somo

la

6

kwa

ajili

ya

Februar

i

9, 2019

Slide2

Nikamwambia, Bwana wangu, wajua wewe. Akaniambia, Hao ndio wanatoka katika dhiki ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao, na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-Kondoo.’” (Ufunuo 7:14, SUV)

FUNGU

KIONGOZI

Slide3

Pepo 4. Ufunuo

7:1-3

144,000 waliotiwa muhuri. Ufunuo 7:4-8Mkutano Mkubwa. Ufunuo 7:9-17Malimbuko ya wasiotiwa unajisi. Ufu. 14:1-4Bila uongo wala mawaa. Ufunuo 14:5Watu 144,000 waliotiwa muhuri wanawakilishwa katika sura mbili: Ufunuo 7 na 14:1-5.Katika sura ya kwanza, wanasimama kwa sababu Mwana-kondoo Anakuja. Katika ile ya pili, wamekataa kupokea chapa ya mnyama.Wanakamilisha hesabu ya waliokombolewa—wale waliotiwa muhuri kwa ajili ya wokovu—, kutano la watu “wa kila taifa, kabila, lugha, na jamaa.”

Slide4

PEPO 4

akisema, Msiidhuru nchi, wala bahari, wala miti, hata tutakapokwisha kuwatia muhuri watumwa wa Mungu wetu juu ya vipaji vya nyuso zao.” (Ufunuo 7:3)Katika unabii, pepo huwakilisha vita kati ya mataifa (Danieli 7:2). Mungu anaweza kuzitumia kubeba hukumu zake (Yeremia 51:1).Mungu hatamruhusu Shetani kuonyesha nguvu zake zote za uharibifu hadi pale watu wa Mungu watakopokuwa wametiwa muhuri (Ezekieli 9:1-11).Muhuri hutumika kutambulisha umiliki wa Mungu (2Tim. 2:19). Watu wa Mungu wametiwa muhuri na Roho Mtakatifu katika historia yote ya wanadamu (Waefeso 1:13-14).Katika siku za mwisho, wale watunzao amri za Mungu na kumwabudu katika siku aliyoitakasa watatiwa muhuri (Uf. 14:12).

Slide5

144,000 WALIOTIWA MUHURI

Nikasikia hesabu yao waliotiwa muhuri katika kila kabila ya Waisraeli, watu mia na arobaini na nne elfu.” (Ufunuo 7:4)144,000 ni namba ya kiishara. Kama ingekuwa namba halisi, basi 144,000 wangekuwa wanaume wa kiyahudi pekee ambao hawakutenda dhambi. Kulingana na Paulo, hilo haliwezekani (Warumi 3:23).Kabila la Dani halijahesabiwa kwa sababu ya ibada zao za sanamu (Waamuzi 18). Efraimu naye amebadilishwa na baba yake Yusufu, labda ni kwa sababu ya ibada ya sanamu pia (Hosea 4:17).Nani na jinsi gani tunavyoabudu ni muhimu ili kujua nani atatiwa muhuri.12x12 huwakilisha watu wa Mungu kutoka Agano la Kale na Agano Jipya. 1,000 hutumika katika fasihi za Kiebrania kuwakilisha “wengi” (Kumb. 32:30; 1Sam. 18:7; Isa. 60:22).

Slide6

MKUTANO MKUBWA

Baada ya hayo nikaona, na tazama, mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele za Mwana-kondoo, wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao.” (Ufun. 7:9)Kama ilivyo katika sura zingine, Yohana alisikia na badaye alionao (Uf. 1:10, 12; 5:5, 6; 9:6, 7). Yohana aliwaona wote waliokombolewa.Wale wa mwisho kutiwa muhuri ni miongoni mwao, kundi lijulikanalo kama “144,000.” Wote waliokombolewa walipokea tuzo kwa wakati mmoja (Waebrania 11:39-40).Kwanini wako mbele ya kiti cha enzi na Mwana-kondoo?Kwa sabau “wamefua mavazi yao, na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-kondoo.” (Uf. 7:14)Wamepigania imani, lakini watasimama pale kwa sababu tu wamepokea haki ya Kristo kwa neema.

Slide7

MALIMBUKO YA WASIOTIWA UNAJISI

Hawa ndio wasiotiwa unajisi pamoja na wanawake, kwa maana ni bakira. Hawa ndio wamfuatao Mwana-kondoo kila aendako. Hawa wamenunuliwa katika wanadamu, malimbuko kwa Mungu na kwa Mwana-kondoo.” (Ufunuo 14:4)Wale ambao hawakutiwa unajisi pamoja na wanawake wamesimama mbele ya Mwana-kondoo. Mwanamke ni Babeli na binti zake (Uf. 17:5).Katika siku za mwisho, lile kundi la watu ambao hawakupotoshwa na makanisa potofu. Na kama sasa wako Babeli, watatoka kwake (Uf. 18:1-4).Wao ni malimbuko, mazao mazuri kutoka katika mavuno yaliyotolewa kwa Mungu (Hesabu 18:12).Wao ni kundi maalumu kwa sababu watabadilishwa katika marejeo ya pili bila kufa.Watatunza uaminifu wao kwa Mungu hadi mwisho. Hao “wazishikao amri za Mungu na imani ya Yesu.” (Uf. 14:12)

Slide8

BILA UONGO WALA MAWAA

Na katika vinywa vyao haukuonekana uongo. Maana hawana mawaa mbele ya kiti cha enzi cha Mungu.” (Ufunuo 14:5KJV)Hilo halimanishi kuwa hawakutenda dhambi, lakini kila doa la dhambi limeondolewa kwa sababu wao “wamefua mavazi yao… katika damu ya Mwana-kondoo.”Hawana waa kama Ibrahimu na Ayubu walivyokuwa (Mwanzo 17:1; Ayu 1:1). Katika vizazi vyote, Mungu amekuwa nao wanaume na wanawake ambao wamekuwa sehemu ya kanisa “lisilo na ila, wala kunyanzi, wala lolote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa.” (Waefeso 5:27)Tabia zetu zitaaksi tabia ya Yesu kama tutajishikamanisha katika Neema na Msamaha wake kwa imani (2 Wakorintho 3:18).Unawezapia kuwa sehemu ya kundi hilo maalumu.

Slide9

“Moja ya alama muhimu katika uwepo wa 144,000 ni kwamba katika vinywa vyao haikuonekana hila. Bwana amesema, “Heri mtu yule...ambaye katika roho haikuonekana hila.” Wanakiri kuwa watoto wa Mungu, na wanaonekana kuwa wakimfuata Mwana-kondoo kila aendako. Na wameonekana mbele yetu kama wemesima katika mlima Sayuni, wakiwa katika mfumo wa huduma takatifu, wamevikwa nguo nyeupe, ambayo ni haki ya watakatifu. Lakini wote watakaomfuata Mwana-kondoo mbinguni ni lazima kwanza wawe wamemfuta duniani, katika ukweli, upendo, utii, wakimfuata bila hasira wala kubadilika, lakini kwa ujasiri, uaminifu, kama kondoo wakimfuata mchungaji wao.

E.G.W. (Selected Messages, vol. 3, cp. 57, p. 424)

Slide10

“Wale wote ambao

majina

yao hatimaye yataonekana kwenye kitabu cha uzima cha Mwana-kondoo watalipigania kiume pambano la Bwana. Watafanya kazi kwa bidii kupambanua na kutupilia mbali majaribu na uovu. Watahisi kuwa jicho la Mungu liko juu yao na kwamba uaminifu mkali unahitajika. Kama waangalizi waaminifu wataendelea kuzuia, kwamba Shetani asije akawapita amejibadilisha kama malaika wa nuru kufanya kazi yake ya mauti kati yao... watafua mavazi yao ya tabia na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-kondoo. Hawa wataimba wimbo wa ushindi katika Ufalme wa utukufu.”E.G.W. (My life today, November 13)

Related Contents


Next Show more