Malengo ya Mafunzo Kuelewa mbinu kuu za utoaji ushauri Kujifunza na kutumia vyombo vya mahojiano ya kutia motisha katika kutoa ushauri wa kuzingatia matumizi ya dawa Mukhtasari Mbinu Kuu za Utoaji Ushauri ID: 830260
Download The PPT/PDF document "Modyuli ya 2: Kuunga Mkono Mabadiliko y..." is the property of its rightful owner. Permission is granted to download and print the materials on this web site for personal, non-commercial use only, and to display it on your personal computer provided you do not modify the materials and that you retain all copyright notices contained in the materials. By downloading content from our website, you accept the terms of this agreement.
Slide1
Modyuli ya 2:
Kuunga Mkono Mabadiliko ya Tabia
Slide2Malengo ya Mafunzo
Kuelewa mbinu kuu za utoaji ushauri
Kujifunza na kutumia vyombo vya mahojiano ya kutia motisha katika kutoa ushauri wa kuzingatia matumizi ya dawa
Slide3Mukhtasari
Mbinu Kuu za Utoaji Ushauri
Ushirikiano wenye Uaminifu baina ya Mgonjwa na Mshauri
Elimu ya Afya yenye Ushirikiano
Mahojiano ya Kutia Motisha
Slide4Ushirikiano wenye Uaminifu baina ya Mgonjwa na Mshauri
Slide5Ushirikiano wenye Uaminifu baina ya Mgonjwa na Mshauri
Kuangaliana uso kwa uso
Kumwangalia mtu ana kwa ana ni njia ya kwanza ya kuwaonyesha kwamba wao ni muhimu na unawajali
Usitazame ubao wa karatasi au hati wakati mtu anapozungumza.
Wakati wa kutoa ushauri, zingatia kile ambacho mtu anasema na uonyeshe umakini kwa kutumia ishara za mwili.
Tingiza kichwa kukubali kuonyesha umeelewa kilichosemwa.
Uliza maswali ya kufuatilia ili kupata ufafanuzi: “Ningetaka kufahamu vyema, unaweza kunifafanulia zaidi?
Kuangaliana uso kwa uso
Kusikiliza Mgonjwa kwa Makini
Slide6Ushirikiano wenye Uaminifu baina ya Mgonjwa na Mshauri
“Watu wengi huwa na shida ya kutumia dawa za kudhibiti VVU (ARV) kila siku.”
“Asante kwa kuniarifu ili tusaidiane kuifanya liwe jambo rahisi.”
Kwa ishara za mwili
Kuinama mbele wakati mtu amekasirika, au kumpa kitambaa cha kujipanguza machozi
Ishara za uso: kutohukumu na kuwa na huruma
Kwa maneno
“Nasikia jinsi ilivyokuwa vigumu kufanya hivyo, samahani ilibidi uyapitie hayo.”
“Unatia bidii sana, naona una mengi sana ya kufanya.”
Kuonyesha kuwa Unajali
Kufanya tatizo kuwa Jambo la Kawaida na Kutohukumu
Slide7Ushirikiano wenye Uaminifu baina ya Mgonjwa na Mshauri
Onyesha kuwa unawatakia mema
“Lengo langu leo ni kukusaidia kudhibiti hali yako ya afya.”
“Ningependa tuwaze pamoja jinsi ya kuboresha mambo yako.”
Iwapo watakuambia jambo ambalo ni ngumu, waonee huruma.
Mgonjwa: “Sijakuwa nikitumia dawa zangu.”
Mtoaji Huduma: “Asante kwa kunifahamisha hili, ni vigumu kulizungumzia lakini nakushukuru kwa kuniamini na kuniambia hili. Hebu tuzungumze jinsi ya kusaidiana kuboresha afya yako.”
Mgonjwa: Sina uhakika kuwa nina VVU, najihisi vyema wakati sijatumia dawa zangu.”
Mtoaji Huduma: “Nina furaha sana umelizungumzia hilo. Hebu tuzungumzie yanayokutatiza.”
Kukuza Uaminifu
Slide8Ushirikiano wenye Uaminifu baina ya Mgonjwa na Mshauri
“Je, una imani ni nini kitakuwa bora kwako katika siku za usoni?”
“Umesema kwamba watoto ndio jambo la muhimu sana kwako, kuwa na afya njema kunawezaje kuwasaidia watoto wako?”
“Unafikiri ni nini kinaweza kuwa bora kwako ikiwa ungekuwa unatumia dawa zako?”
“Ninaona una nguvu ya kukabiliana na changamoto nyingi sana, na nina uhakika tunaweza kushirikiana kukusaidia kutumia dawa zako.”
“Una motisha sana ya kuwa na afya njema kwa ajili ya watoto wako, kutumia dawa ipasavyo kutakuwezesha kuwa na nguvu na afya.”
Malengo ya Mtu Binafsi
Kutia Matumaini
Slide9Ushirikiano wenye Uaminifu baina ya Mgonjwa na Mshauri
Iwapo unahisi kuwa mtu fulani anahitaji usaidizi zaidi ya ule ambao unaweza kutoa, tafuta msaada wa ziada na mwongozo.
Toa tu usaidizi unaowezekana ili kuepuka kupoteza uaminifu wako kwa mgonjwa
Kujua Mipaka Yako
Slide10Kufanya tatizo kuwa Jambo la Kawaida na Kutohukumu
Uzingatiaji wa matumizi ya dawa ni tatizo linalowakumba watu wengi kwa sababu si rahisi.
Si kwamba wewe ndiye dhaifu, tatizo ni kuwa jambo lenyewe ni ngumu.
Slide11Kufanya tatizo kuwa Jambo la Kawaida na Kutohukumu
Karibu kila mtu hukosa kutumia vipimo vinavyohitajika vya dawa. Tunahitaji kuwasaidia watu kuwa na utulivu wanapozungumza kuhusu tukio hili ambalo ni la kawaida.
Kutozingatia vipimo vya dawa huhatarisha afya ya wagonjwa. Watoaji huduma za afya hawaumizi na kutozingatia kwa hivyo hatupaswi kukasirika au kuudhika.
Slide12Kufanya tatizo kuwa Jambo la Kawaida na Kutohukumu
Watu wengi huwa na shida ya kutumia dawa za kudhibiti VVU (ARV) kila siku.
Uliza maswali ambayo yanaashiria kwa uwazi kuwa unatarajia mgonjwa alikosa vipimo vya dawa kwa sababu hili jambo la kawaida:
“Niambie kuhusu kipimo cha mwisho cha dawa ambacho ulikosa?”
“Mara yako ya mwisho ya kukosa kipimo cha dawa ilikuwa lini?”
“Ni nini huwa kikwazo wakati unapokosa kutumia kipimo cha dawa?”
Slide13Kufanya tatizo kuwa Jambo la Kawaida na Kutohukumu
Sifu juhudi, sio matokeo. Hii itapunguza udanganyifu wa kuripoti uzingatiaji wa kiwango cha juu ili wagonjwa wasikuvunje moyo.
“Hilo ni jambo zuri sana kwamba
unajaribu
kutumia dawa zako kila siku.”
“Idadi yako ya virusi iko chini, lazima uwe
unajaribu sana
kutumia dawa zako za kudhibiti VVU (
ARV).”
Slide14Kufanya tatizo kuwa Jambo la Kawaida na Kutohukumu
Idadi ya Virusi ni ya juu
Je, ni zipi baadhi ya njia za kutoa maoni?
Slide15Kutoa Elimu ya Afya kwa Ushirikiano
Una taarifa nyingi na unataka kusaidia watu waelewe afya yao.
Kutoa taarifa kwa njia ya majadiliano badala ya mhadhara kuta:
Dumisha uhusiano wenye uaminifu kati yako na mgonjwa
Hakikisha mgonjwa anapokea taarifa unazompa kwa njia inayofaa
Kadiria yale ambayo mgonjwa anajua
Lenga taarifa ambazo mgonjwa anahitaji
Boresha motisha ya mgonjwa ya kujifunza taarifa hiyo
Saidia watu kudhibiti afya yao wenyeweMaswali huendeleza majadiliano
na yatahimiza mgonjwa pia kuuliza maswali pale ambapo haelewi.
Slide16Kutoa Elimu ya Afya kwa Ushirikiano
Slide17Kutoa Elimu ya Afya kwa Ushirikiano
Uliza
Thibitisha
Uliza
Fahamisha
Uliza
“Watu wengi huwa na changamoto kutumia dawa za kudhibiti VVU kwa vipimo vinavyotakikana. Je, unaona ni nini huwa ngumu sana kwako?”
“Nadhani hilo huvunja moyo sana. Mara nyingi watu hukwambia kufanya jambo ambalo hutaki, ni vigumu kulikumbuka, na halionekani kuwa la muhimu.
“Je, ungependa kupata maelezo zaidi kuhusu kwa nini kutumia dawa za kudhibiti VVU hukufanya uwe na afya?”
Zingatia sana faida zinazoonekana haraka kama kudumisha wapenzi wakiwa na afya njema, ziara chache za hospitali, kudumisha afya ya mwili na akili, na kuwa na dawa chache za kutumia
.
“
Je, una maswali yapi kuhusu taarifa hiyo niliyokupa?”
“Je, kuna moja kati ya faida nilizokutajia ambayo unaona inaweza kuwa muhimu kwako?”
“Je, kuwa na ufahamu wa taarifa hii kunabadilishaje mawazo yako kuhusu dawa za kudhibiti VVU?”
Slide18SHUGHULI
Wakufunzi wataonyesha jinsi ya kutoa elimu ya afya yenye ushirikiano kwa kujadili kuhusu idadi ya virusi.
Slide19Utangulizi wa Mahojiano ya Kutia Motisha
Slide20Mahojiano ya Kutia Motisha
Kufikia Watu Katika Hali Zao
Tunataka kufanya kazi na wagonjwa, sio kuwapinga.
Matukio ya maisha, stadi, na maarifa huathiri utayari kwa mabadiliko.
Ikiwa mtoa huduma anafanya juhudi za kupanga malengo na mtu ambayo hajajitolea kubadilika, hali hii inaweza kupelekea mvutano baina yako na mgonjwa wako.
Dalili zinazoashiria kuwa kuna uwezekano wa kutoelewana na mgonjwa wako:
Unajikuta ukifanya juhudi nyingi za kumhakikishia mgonjwa jambo fulani
Unabishana na mgonjwa
Unaposhuhudia ishara hizi, ni muhimu kukoma kubishana na mgonjwa na badala yake kufanya kazi katika kiwango chake/kasi yake cha mabadiliko.
Slide21Mahojiano ya Kutia Motisha:
Kuongeza Motisha ya Kubadilika
Mbinu zinazofuata zinaweza kuongeza motisha ya kubadilika na kukuza haliza ushirikiano:
Slide22Mahojiano ya Kutia Motisha:
Kuongeza Motisha ya Kubadilika
Maswali Yanayohitaji Majibu Wazi:
Epuka kuuliza maswali yenye majibu ya Ndiyo/Hapana
“Je, nini hufanya iwe vigumu kwako kutumia dawa za kudhibiti VVU kila siku?”
“Je, umefanya nini tayari ili kujaribu kutumia dawa zako za kudhibiti VVU kila siku?”
“Je, unafikiri ni nini kinaweza kufanyika ikiwa utaendelea kutumia dawa zako za kudhibiti VVU kama unavyotumia sasa?”
Slide23Mahojiano ya Kutia Motisha:
Kuongeza Motisha ya Kubadilika
Uthibitisho:
Sifia Juhudi za Kubadilika
“Ninashukuru kwamba unaweza
kuwa mkweli kuhusu jinsi unavyotumia dawa zako za kudhibiti VVU.”
“Bila shaka una uwezo wa
kumudu changamoto nyingi sana.”
“Umetia bidii sana
kutumia dawa zako licha ya changamoto hizi.”
Slide24Mahojiano ya Kutia Motisha:
Kuongeza Motisha ya Kubadilika
Kusikiliza kwa Makini:
Rudia walichokuambia
“Unashangaa ikiwa
kuna faida za kutumia dawa za kudhibiti VVU.”
“Ulisema kwamba
unahuzunika unapowaza kuhusu kutumia dawa za kudhibiti VVU na hilo hufanya uzingatiaji kuwa mgumu sana.”
“Nilichosikia ukisema ni kwamba una mambo mengi yanayokusukuma, na hivyo dawa zako si jambo la muhimu sana kwa sasa.”
Slide25Mahojiano ya Kutia Motisha:
Kuongeza Motisha ya Kubadilika
Kauli za Mukhtasari
“Hebu nione kama nimekuelewa kufikia sasa.
Una matatizo ya kutumia dawa zako za kudhibiti VVU ipasavyo kwa sababu ingawa unataka kuhisi vyema na kuwa na afya njema, una matatizo mengine pia ambayo yanafanya iwe vigumu kuzingatia afya yako.”
“Nimesikia ukisema hivi, hebu niambia kama mimekuelewa sawa.
Unajihisi vizuri hata unapokosa kipimo cha dawa na huna uhakika iwapo dawa za kudhibiti VVU ni muhimu ili kudumisha afya yako.”
Slide26SHUGHULI
Jiunge na mwenzi na mbadilishane majukumu katika kuigiza mgonjwa na mtoaji huduma kwa kutumia Grace na John kama wahusika. Tumia stadi za OARS ili kujadili matatizo ya mhusika katika kuzingatia matumizi ya dawa za kudhibiti VVU.
Slide27Grace
Ana umri wa miaka 28
Aligundua kuwa ana VVU miaka 3 iliyopita alipokuwa na mimba ya bintiye mchanga.
Ana watoto watatu (wenye umri wa miaka 8, 6, na 3) ambao wote hawana VVU.
Alitumia dawa vizuri alipokuwa na mimba na akinyonyesha lakini sasa anaona ugumu kuzitumia ipasavyo.
Slide28John
Ana umri wa miaka 36
Aligunduliwa kuwa ana VVU kwa mara ya kwanza miaka 10 iliyopita
Hutia bidii kumudu mahitaji ya familia yake (bibi na watoto wawili, wenye umri wa miaka 10 na 7)
Hajatumia dawa zake inavyofaa kwa zaidi ya miezi kadhaa na hajakuwa na matatizo yoyote ya kiafya kufuatia hilo
Slide29Mjadala: Mahojiano ya Kutia Motisha
Je, ni nini kilikuwa ngumu kuhusu kutumia stadi hizi?
Je, ni nini kilikuwa tofauti kuhusu jawabu la mwenzio la swali linalohitaji jibu wazi?
Je, ulihisiaje kauli yako ilipothibitishwa?
Je, ni nini kilifanya uthibitisho au tafakari kutokea kama ya kweli (au isiyo ya kweli)?
Je, kauli za mukhtasari zilionekanaje zenye faida?
Slide30Mukhtasari
Kubali
: Kuwa na mtazamo wa kutohukumu kuhusiana na mabadiliko ya tabia.
Shirikiana:
Kabla ya kutoa elimu ya kisaikolojia, maswali ni muhimu ili kumhusisha mtu katika mafunzo.
Tia Motisha
: Kuzingatia na kufanya kazi na mtu katika hali yake kwa kuonyesha unamuelewa kunaweza kuchochea na kusaidia katika kujipa motisha.
Kumbuka kutumia mbinu za OARS!
Slide31Una Maswali?